Leokadia wa Toledo (Toledo, Hispania, karne ya 3 - Toledo, 9 Desemba 304) alikuwa bikira Mkristo aliyeuawa katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano akiacha ushuhuda maarufu wa imani yake kwa Yesu [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.