Leucho wa Brindisi, mzaliwa wa Aleksandria, alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo wa Italia Kusini katika karne ya 4.
Kabla ya hapo alikuwa mmonaki katika nchi yake, Misri.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Januari[1].