Liturujia ya Mesopotamia ni liturujia maalumu yenye asili katika Mesopotamia ya kale, ambayo kimapokeo inatajwa kama imetokana na Mtume Thoma, na inatumiwa hasa na Wakristo Waashuru na Wakaldayo wa Iraq na nchi za kandokando, pamoja na Wamalabari wa India kusini, wengi wao wakiwa Wakatoliki na waliobaki Waorthodoksi wa Mashariki, ambao wote wametokana na wale waliotengwa na Mtaguso wa Efeso (431).[1][2] Kwa jumla ni milioni 5 hivi pamoja na wale waliotawanyika karibu duniani kote.
Hata matoleo ya vitabu vya liturujia hiyo kwa kiasi kikubwa yamefanywa na Wakatoliki. Lugha yake hasa ni Kiaramu.