Liturujia ya Misri

Picha takatifu ya Kimisri ya Mwinjili Marko, mwanzilishi wa Kanisa la Aleksandria. Jina rasmi la liturujia hiyo ni Liturujia ya Mt. Marko.

Liturujia ya Misri ni liturujia asili ya Wakristo wa Misri ambayo kutoka jiji la Aleksandria ilienea hasa Ethiopia na Eritrea.

Inatumiwa na Kanisa la Kiorthodoksi la Misri, na vilevile na Kanisa Katoliki la Kimisri, pamoja na makanisa dada ya Ethiopia, Eritrea n.k. na kokote walikohamia Wakopti.

Wataalamu wanatambua uhusiano wa pekee kati ya liturujia hiyo na ile ya Roma, kwa mfano katika muundo wa anafora, ingawa ni ya mashariki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne