Lugha za Kiaustronesia

Uenezaji wa lugha za Kiaustronesia duniani

Lugha za Kiaustronesia ni familia ya lugha ambazo huzungumzwa katika visiwa vya Pasifiki, vya Asia ya Kusini-Mashariki na kisiwa cha Madagaska. Katika familia hiyo kuna lugha zaidi ya 1200 zenye wasemaji milioni 386.

Lugha ya Kiaustronesia yenye wasemaji wengi zaidi ni Kimalay ambayo huzungumzwa na watu milioni 180.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne