Lugha za Kihindi-Kiulaya ni jamii ya lugha iliyo kubwa kuliko zote duniani. Imekadiriwa kuna lugha hai 445 za jamii hiyo na wasemaji bilioni 3.2 katika mabara yote (46% za watu wote wa leo).
Uenezi huo umetokana hasa na historia ya ukoloni wa Kizungu uliopeleka lugha za Ulaya pande zote za dunia.
Lugha zenye wasemaji zaidi ya milioni 100 ni: Kihispania, Kiingereza, Kihindustani (Kihindi/Kiurdu), Kireno, Kibengali, Kipanjabi na Kirusi.
Nyingine zenye wasemaji zaidi ya milioni 50 ni: Kijerumani, Kifaransa, Kimarathi, Kiitalia na Kiajemi.