Lugha za Kihmong-Mien ni familia ya lugha ambazo huzungumzwa katika Asia ya Kusini-Mashariki, hasa nchini Uchina, Vietnam na Laos. Idadi ya lugha katika familia hiyo ni 20 takriban. Zamani lugha za Kihmong-Mien zilifikiriwa kuwa tawi la lugha za Kisino-Tibeti lakini siku hizi zinaaminiwa kuwa familia tofauti yenyewe.