Lushoto | |
Mahali pa mji wa Lushoto katika Tanzania |
|
Majiranukta: 4°46′48″S 38°16′48″E / 4.78000°S 38.28000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Tanga |
Wilaya | Lushoto |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 21,870 |
Lushoto ni mji mdogo uliopo kwa kimo cha mita 1930 juu ya UB kwenye milima ya Usambara na ni makao makuu ya wilaya ya Lushoto.
Kiutawala ni kata moja tu na kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 28,190 waishio humo. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 21,870 [1].
Kuna barabara ya lami kati ya Lushoto na Mombo inapounganika na barabara kuu B1 Arusha - Dar es Salaam.
Mazingira ya Lushoto yanafaa kwa kilimo; pia kuna vivutio vya utalii.