Lusori

Sanamu yake iliyotengenezwa na Donatello ili kutunza masalia yake.

Lusori (pia: Luxurius, Luxorius, Ruxurius, Ruxorius, Rossore; alifariki Forolongianus katika kisiwa cha Sardinia, leo nchini Italia, 21 Agosti 304) alikuwa askari wa Dola la Roma ambaye aliongokea Ukristo akauawa kwa hiyo imani yake mpya wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini[2].

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[3].

Pengine wanatajwa kama wenzake watoto Siselo na Kamerino.

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91001
  2. A marble Latin inscription dating to the 6th century built into the south side of san Lussorio church about 1.5 km from Fordongianus attests to his cult at that date: "(H)ic effusus est sangu(is) / beatissimi martyris / Luxuri. Celebratur / natale eius XII c(a)l(enda)s S(e)p(tem)b(re)s / renobatu(r) sup temporibus Helia(e) ep(is)c(o)p(i)." In 599 Gregory the Great should have wrote a letter to Januarius, bishop of Cagliari, referring to a monastery dedicated to saints Gavinus and Luxurius, probably in Cagliari itself, showing the spread of Luxurius' cult across Sardinia. He is the patron saint of several Italian cities.
  3. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne