MURS | |
---|---|
Murs (kulia) na 9th Wonder wakitumbuiza katika Tamasha za ‘’Paid Dues hip hop’’ at the Ukumbi wa Nokia Jijini New York.
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Nick Carter |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Msanii wa Rap |
Miaka ya kazi | 1996 – leo |
Studio | Warner Bros. Records Definitive Jux Record Collection |
Ame/Wameshirikiana na | Living Legends, Felt, 9th Wonder, 3 Melancholy Gypsys, The Invincibles |
Tovuti | www.mursmusic.com/ |
Nick Carter (ambaye anajulikana kwa jina la usanii kama MURS) ni msanii wa Marekani wa muziki wa aina ya Rap. Jina lake la kisanii la MURS ambalo aliliunda mwenyewe linaweza kuwa na maana nyingi kama vile "Making the Universe Recognize and Submit" au "Making Underground Raw Shit"[1] Alitia mkataba wa lebo ya kibinafsi ya Record Collection na ni mwanachama wa Makundi ya Muziki aina ya Hip Hop ya Living Legends, Felt na 3 Melancholy Gypsys. MURS pia ni mwanabendi wa bendi ya muziki wa aina ya Punk Fusion iitwayo The Invincibles pamoja na Jacksonville, ambaye hujiita Mkate wa Ngano (Whole Wheat Bread) kutoka Florida, ambapo anaimba sauti ya Lead.