Maada kwa kawaida inaweza kupatikana katika hali nne. Picha zinazionyesha kutoka juu kwenda chini: kwazi (mango), maji (kiowevu), daioksidi ya nitrojeni (gesi), na tufe la plazma (plazma). |
Maada (kutoka Kiarabu; pia: mata kutoka Kiingereza matter) ni neno pana linalojumlisha vyote vinavyoweza kuonekana, kusikika, kuguswa, kuchunguzwa n.k., ikiwemo hasa maada ya kawaida inayoundwa na atomi ambazo tena zinaundwa na kiini cha protoni na neutroni, kikizungukwa na wingu la elektroni.[1][2] Hivyo maada ni kitu chochote chenye uzito na kinachoweza kuchukua nafasi.
Tangu karne ya 20 ufafanuzi sahihi wa maada umeshindikana kutokana na maendeleo ya sayansi, nayo si tena jambo la msingi katika fizikia kama ilivyokuwa awali.[3][4]
Maada inapatikana kwa kawaida katika hali nne: mango, kiowevu, gesi na utegili. Maada huweza kubadilika pale tu halijoto inapobadilika. Badiliko la maada linaweza kuwa kutoka gesi kwenda yabisi mfano mvuke kuwa barafu, yabisi kwenda gesi mfano barafu kuwa mvuke, kimiminika kuwa yabisi mfano maji kuwa barafu n.k.
Hivyo matawi mbalimbali ya sayansi yanatumia neno maada kwa maana tofautitofauti.[5][6][7]
Falsafa pia inatumia neno hilo, hasa kwa kutofautisha maada na roho, na hivyo ulimwengu unaoonekana na ule ambao hauonekani, lakini unasadikika kuwepo.
{{cite book}}
: Unknown parameter |editors=
ignored (|editor=
suggested) (help)
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help)