Mac Cairthinn wa Clogher (pia: Aedh, Aidus, McCartan, Macartan; alifariki 506) alikuwa askofu wa kwanza wa Clogher, Eire kuanzia mwaka 454[1].
Inasemekana aliongokea Ukristo kwa juhudi za Patrick wa Ireland.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.