Machweo

Jua, dakika moja kabla ya kuchwa huko Ureno.
Machweo katika Hifadhi ya Taifa Nyerere Tanzania.

Machweo (au Magharibi) ni kipindi cha siku ambapo jua linatoweka kabisa kwa macho ya watu wa eneo fulani, kabla ya kwanza usiku. Kinyume chake ni macheo au pambazuko inayotokea wakati usiku unakwisha na mchana unaanza.

Wakati huo rangi nyekundu inatawala mandhari.

Binadamu na wanyama wengi wakati huo wanakwenda mahali pa kupumzika usiku.

Dini mbalimbali zinaagiza sala kwa wakati huo, kwa mfano Ukristo na Uislamu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne