Mafuta (chakula)

Makorosho yana mafuta mengi mazuri

Mafuta au shahamu ni sehemu za chakula pamoja na wanga, protini na vitamini. Neno "fati" (kutoka Kiing. fat) afadhali lizuiwe. Vyakula vilivyo na mafuta mengi ni k.m. maparachichi, karanga, makorosho, mbegu kama alizeti na siagi.

parachichi
Parachichi

Vyakula hivi humsaidia mtu kwa kumpatia joto hasa wakati wa baridi, pia huchangia katika uzalishaji wa nishati na nguvu kwa ajili ya mwili na pia hufanya kazi mbalimbali katika mmeng'enyo wa chakula tumboni.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne