Magharibi

Alama za dira zikionyesha magharibi katika hali ya mkoozo (W = "West" = magharibi)

Magharibi ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande wa machweo ya jua.

Magharibi ni pia jina la saa ya swala ya jioni ya Waislamu na swala yenyewe.

Jina "magharibi" limetokana na neno la Kiarabu مَغْرِب maghrib linalomaanisha sehemu upande wa machweo.

Magharibi kawaida huwa upande wa kushoto kwenye ramani. Tanzania iko upande wa magharibi wa Bahari Hindi, Burundi iko upande wa magharibi wa Tanzania, na nchi ya Malawi iko upande wa magharibi wa Msumbiji.

Kwa maana ya kiutamaduni kuna mazoea ya kutaja utamaduni wa Ulaya pamoja na Marekani (ambayo ni mtoto wa utamaduni wa Ulaya) kama "ustaarabu wa magharibi", kinyume chake ni "mashariki" kwa maana ya Asia.

Wakati wa vita baridi magharibi ilikuwa kifupi cha nchi za kibepari zilizofuata mtindo wa demokrasia kinyume na mashariki iliyomaanisha nchi za kikomunisti.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne