Maigizo

Mwigizaji wa jukwaani wa awali kabisa, Sarah Bernhardt, akicheza kama Hamlet.

Maigizo (kwa Kiingereza: drama, kutoka Kigiriki: δράμα, dráma) ni mpangilio wa maneno unaombatana na utendaji wa wahusika. Wahusika huwa wanaiga mambo ambayo yanafanywa na jamii husika na kuyaonesha mbele ya hadhira. Pia maneno yanayosemwa na wahusika yanalingana na yale ya jamii husika.

Hivyo basi katika sanaa hii hutumika vitendo, misegeo/mijongeo ya mwili na miondoko mbalimbali kwa umbo lenye kuvutia hadhira. Wakati mwingine maigizo huambatana na nyimbo. Utanzu wa maigizo hujumuisha vipera kama vile: matambiko, majigambo, ngonjera, ngoma, vichekesho, michezo ya jukwaani na kadhalika.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne