Mainchin (kwa Kieire: Mainchín mac Setnai; alifariki Limerick, Ireland, mwishoni mwa karne ya 6 au mwanzoni mwa karne ya 7) anasemekana kuwa askofu wa mji huo. Jina lake linamaanisha "Mmonaki mdogo"; aliitwa pia "Mwenye hekima"[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.