Maisha ya kiroho

Kuungana na Kristo ndiyo lengo la maisha ya Kiroho.


Maisha ya Kiroho katika Ukristo ndiyo maisha ya kuongozwa na Roho Mtakatifu nyuma ya Yesu Kristo kwa utukufu wa Mungu Baba.

Ufuasi huo unafanyika pamoja na waamini wengine katika Kanisa, jumuia ya wanafunzi wa Yesu inayotokana na kundi la kwanza, lililoundwa na Mitume wake.

Mwanzo wake wa kawaida ni ubatizo, uliofananishwa na Yesu mwenyewe na aina ya kuzaliwa upya kwa maji na Roho Mtakatifu.

Uzima huo mpya unalishwa mfululizo na Neno la Mungu na ekaristi.

Lengo ni kufikia muungano na Mungu katika uzima wa milele, lakini huo unaanzia hapa duniani katika ustawi wa maadili makuu ya imani, tumaini na upendo, pamoja na vipaji vya Roho Mtakatifu.

Ni hasa neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ingawa juhudi za mhusika zinadaiwa vilevile.

Teolojia hiyo ya maisha ya kiroho ya Kikristo inaitwa pia kifupi Teolojia ya Kiroho.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne