Makumbusho ya Kapenguria

Makumbusho ya Kapenguria ni makumbusho yanayopatikana Kapenguria, kaunti ya Pokot Magharibi, Kenya.[1].

Makumbusho hayo hupatikana katika gereza lililotumika kuwafunga wapigania uhuru wa Kenya kati ya mwaka 1952 na 1953 wakiwemo Jomo Kenyatta, Kungu Karumba, Fred Kubai, Paul Ngei, Bildad Kaggia na Ramogi Achieng Oneko. Vyumba walivyofungiwa mashujaa hao sita, vinatumika kama sehemu ya makumbusho hayo.

Makumbusho hayo yalifunguliwa rasmi mwaka 1993.

  1. "Kapenguria - Location and Historical Background". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-18. Iliwekwa mnamo 2013-04-09. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne