Malcolm X | |
---|---|
![]() Malcolm X mnamo Machi 1964 | |
Amezaliwa | Malcolm Little Mei 19, 1925 |
Amekufa | Februari 21, 1965 (umri 39) Manhattan, New York |
Sababu ya kifo | Kauawa kwa risasi |
Majina mengine | el-Hajj Malik el-Shabazz (الحاجّ مالك الشباز) |
Kazi yake | Minister, activist |
Asasi | Nation of Islam, Muslim Mosque, Inc., Organization of Afro-American Unity |
Ndoa | Betty Shabazz (m. 1958–present) |
Watoto | Attallah Shabazz Qubilah Shabazz Ilyasah Shabazz Gamilah Lumumba Shabazz Malikah Shabazz Malaak Shabazz |
Wazazi | Earl Little Louise Helen Norton Little |
Saini | [[File:{{{signature}}}|150px|alt=]] |
Malcolm X (jina lake la awali lilikuwa Malcolm Stuart Little; baadaye alifahamika kama Hajj Malik; 19 Mei 1925 - 21 Februari 1965) alikuwa mwanaharakati wa Haki za binadamu za Waafrika-Waamerika na haki za kiraia kwa jumla
Malcolm katika kipindi chote cha ukuaji wake aliishi kwa ndugu baada ya kifo cha baba yake na mama yake kwenda kuishi hospitali kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Alijihusisha na shughuli za uhalifu katika maisha yake ya awali na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani mwaka 1946 kwa makosa ya uvunjaji na wizi. Akiwa gerezani alijiunga na Taifa la Uislamu na hapo ndipo alipojipachika jina Malcolm X akimaanisha jina lake la Kiafrika ambalo hakupatiwa kutokana na athari za utumwa. Baada ya kuachiwa toka gerezani mwaka wa 1952 kwa kuonesha tabia njema, kwa haraka sana alipata kuwa mtu mashuhuri ndani ya Taifa la Uislamu.