Mamalia wa majini ni mamalia ambao wanaishi na kupata riziki zao (zote au sehemu) majini, ama baharini ama katika maziwa, mito. Ni wanyama wa spishi mbalimbali (129) jamii ya mamalia ambazo hazihusiani kwa asili, ila zimefuata njia zinazofanana kidogo katika kuzoea kwa kiasi tofauti mazingira hayo badala ya kuendelea kuishi katika nchi kavu[1][2].