Sehemu ya mfululizo wa makala kuhusu mapendo |
![]() Moyo katika mapokeo ya Ulaya ni mchoro unaowakilisha mapendo. |
Vipengele Msingi |
---|
Mapendo kadiri ya sayansi |
Mapendo kadiri ya utamaduni |
Upendo (fadhila) |
Upendo safi |
Kihistoria |
Mapendo ya kiuchumba |
Mapendo ya kidini |
Aina za hisia |
Mapendo ya kiashiki |
Mapendo ya kitaamuli |
Mapendo ya kifamilia |
Mapendo ya kimahaba |
Tazama pia |
Mafungamano ya binadamu |
Jinsia |
Tendo la ndoa |
Maradhi ya zinaa |
Siku ya wapendanao |
Mapenzi ni neno la Kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia, kuanzia mahaba, pendo hadi upendo wa Kimungu.
Ni kwamba kitenzi "kupenda" kinaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofautitofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu ("Napenda chakula hiki"), hadi mvuto mkali kati ya binadamu ("Nampenda mume wangu"). Uanuwai wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi, hata kulingana na hali nyingine za kihisia.
Kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mwingine, yakishirikisha hisia tofauti, kutoka hamu na urafiki wa kimahaba hadi ukaribu wa kihisia wa kifamilia na kitaamuli, usioelekea kabisa ngono[1] na hata umoja wa kina au ibada ya upendo wa kidini. [2]
Mapenzi katika aina zake mbalimbali husimamia mafungamano na, kutokana na umuhimu wake mkuu katika saikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika sanaa.