Mapinduzi (kutoka kitenzi "kupindua" juu chini) ni mabadiliko ya haraka upande wa siasa na miundo yanayotokana na shinikizo la wananchi, linalotumia mara nyingi nguvu.
Katika historia ya binadamu mapinduzi yalitokea mara nyingi kwa sababu, mbinu, muda na malengo mbalimbali.
Hayo yalifuatwa na athari kubwa juu ya utamaduni na uchumi wa jamii husika.
Pengine mabadiliko hayo ya mwisho pia yanaitwa mapinduzi hata yasiposababisha serikali ianguke.