Maria Adolfina Dierk (Osendrecht, Uholanzi, 8 Machi 1866 – Taiyuan, Shanxi, China, 9 Julai 1900) alikuwa sista wa shirika la Wafransisko Wamisionari wa Maria aliyefia dini China alipokuwa mmisionari wakati wa Uasi wa Waboksa.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 119.
Sikukuu yao huadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Julai.