Maria Amandina wa Moyo Mtakatifu

Mt. Maria Amandina.

Maria Amandina wa Moyo Mtakatifu (jina la awali: Paula Jeuris, Schakkebroek, Herk-de-Stad, 28 Desemba 1872Taiyuan, 9 Julai 1900) alikuwa sista wa shirika la Wafransisko Wamisionari wa Maria aliyefia dini China alipokuwa mmisionari wakati wa Uasi wa Waboksa.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 119.

Sikukuu yao huadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Julai.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne