Marinus na Asteri (walifariki Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 262) walikuwa Wakristo ambao walikatwa kichwa kwa sababu ya imani yao chini ya Kaizari Galienus ingawa yeye alikuwa amesimamishwa dhuluma[1] [2].
Marinus alikuwa akida ambaye aliposhtakiwa na askari mwenzake akaungama wazi imani yake mbele ya hakimu akakatwa kichwa [3]. Basi, Asteri, seneta wa Dola la Roma, alitandaza joho lake chini kupokea maiti kwa heshima; kwa ajili hiyo yeye pia akakatwa kichwa hapohapo.
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Machi[4][5].
{{cite book}}
: CS1 maint: unrecognized language (link)