Marselino wa Ancona (alifariki 9 Januari katika karne ya 6) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia ya Kati[1].
Papa Gregori I aliandika askofu huyo alivyookoa mji wake katika hatari ya moto kuuteketeza.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Januari[2].