Martin Luther (10 Novemba 1483 – 18 Februari 1546) alikuwa Mkristo mwanateolojia kutoka nchi ya Ujerumani maarufu kama mwanzilishi wa Uprotestanti.
Kisha kushindana na Papa wa Roma, na kutengwa na Kanisa Katoliki, aliongoza Matengenezo ya Kiprotestanti yaliyosababisha mapema madhehebu mengi mapya kutokana na wazo kuu la kwamba Biblia inajitegemea na kumtosha kila anayesoma.
Aliandika vitabu vingi, kutunga nyimbo kadhaa na hasa kutoa tafsiri maarufu ya Biblia ya Kikristo katika lugha ya Kijerumani.
Athari yake imekuwa kubwa sana katika Kanisa na ulimwengu kwa jumla.