Masalia

Sanduku la kutunzia masalia, yakiwemo ya Mitume wa Yesu na watakatifu wengine.

Masalia ni mabaki ya mwili au ya vitu vya mtu anayeheshimika hasa kwa msingi wa dini.

Masalia ni muhimu hasa katika baadhi ya madhehebu ya dini, kama vile ya Uhindu, Ubuddha na Ukristo.

Katika dini hiyo ya mwisho, heshima kwa masalia ilianza na maiti ya wafiadini, na umuhimu wake ulifikia kilele chake katika Karne za Kati.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne