Masiya (au Masiha), kutoka Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ mashiakh, maana yake Mpakwamafuta ni jina la heshima ambalo Biblia inampa mfalme au kuhani aliyewekwa wakfu kwa Mungu kwa kupakwa mafuta atende kwa niaba yake kazi ya kusaidia taifa lake hasa kwa kulikomboa.[1]
Tofauti na kawaida, Biblia inamtaja kama Masiha hata mfalme Koreshi Mkuu wa Uajemi kwa sababu Mungu alimtumia kutoa Wayahudi katika uhamisho wa Babeli na kuwaruhusu warudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu[2]
Hata hivyo kwa namna ya pekee jina hilo linatumika kwa Mwana wa Daudi, mtawala wa Israeli[3] katika wakati wa mwisho ambao utakuwa wa amani duniani[4]