Mauro wa Parenzo (alifariki Porech, leo nchini Korasya, 305 hivi) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo.
Inasemekana alitokea Afrika Kaskazini na kuwahi kuishi miaka kumi na nane monasterini. Hatimaye aliteswa sana akauawa kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Novemba[2].