Mazinguo (kutoka kitenzi kuzingua, kinyume cha kuzinga; pia: kupunga; kwa Kiingereza: exorcism kutoka Kigiriki: ἐξορκισμός, uapisho) ni dua za kuondoa pepo au viumbe wa kiroho wanaofikiriwa kuleta madhara kwa binadamu au mazingira yake[1].
Vitendo vya namna hiyo vinafanyika toka kale katika dini mbalimbali.
Mtu anayetoa huduma hiyo anaitwa mzinguaji. Katika historia baadhi ya watu wa namna hiyo walipata kuwa maarufu sana, kama vile Yesu.