Mbandaka | |
Mahali pa mji wa Mbandaka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
|
Majiranukta: 0°02.52′0″S 18°15.21′0″E / 0.04200°S 18.25350°E | |
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
---|---|
Mkoa | Mkoa wa Ikweta |
Idadi ya wakazi (2012) | |
- Wakazi kwa ujumla | 345,663 |
Mbandaka ni kati ya miji mikubwa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Iko kwenye ikweta kando ya mto Kongo.
Idadi ya wakazi ni mnamo 200,000. Mbandaka ni makao makuu ya mkoa wa Équateur.
Mji ulianzishwa na mpelelezi Henry Morton Stanley mwaka 1883 kwa jina la Equateurville. Jina likabadilishwa baadaye kuwa Coquilhatville na tangu mwaka 1966 ni "Mbandaka".
Uvuvi ni sehemu muhimu ya uchumi wa mji. Samaki wanauzwa hasa Kinshasa.