Mbinga ni mji katika Mkoa wa Ruvuma nchini Tanzania iliyopata kuwa halmashauri ya pekee mwaka 2015.
Mji huo ulikuwa na kata 20 na wakazi wake walikadiriwa kuwa 140,747 mnamo 2015[1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 158,896 [2].
Mbinga inapitiwa na barabara ya A19 kutoka Songea kwenda Mbamba Bay kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa.
Wenyeji wa Mbinga ni Wamatengo.