Mbio ya Marathoni

Mchoro wa Luc-Olivier Merson unaomuonyesha Fidipide akitangaza ushindi na kufa hapohapo.

Mbio ya Marathoni ni mbio ya masafa marefu kuliko zote, ikichukua kilometa 42.195. Ndiyo kilele cha michezo ya Olimpiki.

Asili ya mchezo huo ni mbio ya urefu huohuo iliyopigwa na Fidipide mwaka 490 KK ili kuwatangazia wananchi wa Athens (Ugiriki) kwamba wamewashinda Waajemi katika mapigano ya Marathon.

Siku hizi wanariadha bora, hasa wa Kenya na Ethiopia, wanafaulu kukimbia umbali huo wote kwa saa 2 na dakika chache tu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne