Mbuni | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Spishi 2, nususpishi 4:
| ||||||||||||
Msambao wa mbuni katika Afrika
|
Mbuni ni ndege wakubwa wa familia Struthionidae. Kuna spishi mbili katika jenasi moja, lakini wataalamu wengine wanafikiri ni spishi moja tu. Ndege hao ni wakubwa kuliko wengine wote. Wana miguu mirefu na shingo ndefu na wanaweza kukimbia sana, hata kwa mwendo wa km 65 kwa saa, lakini hawawezi kuruka hewani.
Rangi za manyoya ya dume ni nyeusi na nyeupe na rangi ya ngozi yake (shingo na miguu) ni nyekundu, pinki au buluu kufuatana na nususpishi. Manyoya ya jike ni kahawiakijivu na rangi ya ngozi ni sawa na dume. Mbuni wanaishi katika savana, nyika na majangwa ya Afrika, lakini wanafugwa ulimwenguni mwote.
Jina la kisayansi la spishi kuu, Struthio camelus, linatoka katika lugha ya Kiyunani: στρουθιον = jurawa na καμηλος = ngamia.
Dume la mbuni ana harimi ya majike 2-7 lakini moja tu anatawala. Dume hupanda majike yote ya harimi yake na majike huyataga mayai yao yote katika tago moja ambalo dume amelitengeneza. Jike anayetawala hutaga kwanza na baadaye hutupa mayai ya majike wasio na nguvu sana. Kwa kawaida hubakisha mnamo mayai 20. Majike huyaatamia mayai mchana na dume hufanya usiku, kwa sababu rangi ya jike inafanana na mchanga na rangi nyeusi ya dume haionekani usiku.