Mchezo wa pool (kwa Kiingereza "Pool" au "Billiards") ni mchezo ambao unachezwa na watu wawili au hata zaidi kwa kutumia mipira minane ya rangi pamoja na mpira mmoja mweupe, pia na fimbo ndefu.
Mchezo huchezwa sana katika nchi za Ulaya na Australia, uwanja wake una vitundu au mifuko sita au nane kwa ajili ya kuingizia mpira.
Mchezo wa pool ni kati ya michezo inayopendwa sana na vijana. Pool huwa na bodi yenye vijishimo ambapo vijana hupiga vijipira kwa miti huku lengo lao likiwa kuweka mipira yote kwa vishimo. Kila mchezaji hujaribu kila awezalo kuhakikisha kwamba yeye ndiye atakayerusha mipira mingi zaidi ndani ya vile vijishimo.