Mgagani | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Migagani
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Migagani, migange, mikabili au miangani ni mimea ya jenasi Cleome katika familia na oda Brassicales (kabichi). Mgagani wa kawaida, Cleome gynandra, huliwa takriban kila mahali pa Afrika na katika mabara mengine pia. Wanawake wengi wenye mimba au waliozaa hula mmea huu, kwa sababu una chuma nyingi kiasi na husaidia kuongeza damu[1]. Mboga ya mgagani huitwa magagani.