Mgeta ni kata na makao makuu ya tarafa ya uwanda wa juu (hadi mita 2,200 na zaidi juu ya UB) katika wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67321.
Ndiyo sehemu ambayo Waluguru wa mwanzo walitokea huko.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 3,789 [1].
Ni sehemu inayosifika sana kwa kilimo cha mboga na matunda, kwa mfano njegere, maharage, mahindi, magimbi na viazi mviringo. Pia ndipo soko kubwa la matunda na mbogamboga lilipo Nyandira.