Mgongo kati wa Atlantiki

Ramani ya mgongo kati ya Atlantiki.

Mgongo kati wa Atlantiki (kwa Kiingereza: Mid-Atlantic Ridge) ni safu ya milima chini ya maji ya bahari ya Atlantiki inayoelekea kutoka 87°N (km 333 kusini kwa Ncha ya kaskazini) hadi kisiwa cha Bouvet kusini mwa dunia kwenye 54°S.

Vilele vya juu vya milima hiyo vinaonekana juu ya UB kama visiwa. Safu hiyo ya milima imetokea mahali ambako mabamba ya gandunia yanaachana: bamba la Ulaya-Asia na bamba la Amerika ya Kaskazini katika Atlantiki ya Kaskazini, halafu bamba la Amerika ya Kusini na bamba la Afrika katika Atlantiki ya Kusini.

Mabamba hayo yana mwendo wa kuachana na katika nafasi kati yake magma hupanda juu inayokuwa mwamba mpya uliosababisha kutokea kwa milima ya safu.

Kutambuliwa kwa safu hiyo kuliweka msingi kwa nadharia ya upanuzi wa misingi ya bahari unaosababisha mwendo wa mabamba ya gandunia.

Faili:Upanuzi msingi bahari.PNG
Magma inapanda juu penye kuachana kwa mabamba ya gandunia na kujenga safu za milima ya migongo chini ya bahari.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne