Mgonjwa

Hii ni picha inayoonesha mgonjwa akiwa hospitali na wanajeshi wamemtembelea.
Mhindi huyu ana njaa, yaani ugonjwa wake umesababishwa na upungufu wa chakula.

Mgonjwa ni mtu aliyeingiliwa na maradhi.

Mgonjwa anapoumwa huonesha dalili mbalimbali za wazi, kwa mfano mgonjwa wa kichwa hushika kichwa. Kuna pia dalili nyingine za ndani ambazo ni muhimu zaidi kwa sababu zinadokeza chanzo cha ugonjwa ambacho ni muhimu kuwahi kupambana nacho.

Mgonjwa huteseka pale ambapo anapoumwa halafu hapewi huduma ya kwanza au hata kumwahisha hospitali. Ni muhimu kuzingatia kwamba kila mtu ana haki ya kuishi, tena vizuri, hivyo ana haki ya kutibiwa.

Pamoja na hayo, utu unadai kumpatia mgonjwa mahitaji yake mengine kwa mwili (chakula n.k.) na kwa nafsi (k.mf. pendo na faraja).

Dini mbalimbali zinaelekeza namna ya kumhudumia hadi mwisho. Kwa mfano Wakristo wa madhehebu mbalimbali wanamuombea na kumpatia sakramenti, zikiwemo kitubio, mpako wa wagonjwa na ekaristi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne