Milburga (jina asili: Mildburh; alifariki 23 Februari 727[1]) alikuwa binti wa ukoo wa kifalme wa Mercia, leo nchini Uingereza[2].
Alikuwa abesi wa monasteri ya Wabenedikto wa Wenlock, maarufu kwa unyenyekevu na miujiza.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana tarehe ya kifo chake.