Mimba ni mtoto wa mamalia ambaye anakua katika tumbo la uzazi la mama yake hadi azaliwe.
Ukuaji huo unaendelea moja kwa moja, bila kupitia hatua zilizo wazi, ingawa pengine lugha zinatumia misamiati tofauti kadiri ya siku au wiki zilizopita tangu mimba itungwe.
Muda wa ukuaji huo wote ni tofauti kadiri ya spishi husika. Kwa binadamu ni miezi 9 hivi.