Minara ya ziwa Jumeirah (Kiarabu ابراج بحيرة الجميرا) ni eneo kubwa la maendeleo huko Dubai, [United Arab Emirates] ambalo lina majumba 79 yalinayojengwa kando mwa maziwa, Manne ya kutengenezwa na binadamu (Ziwa Almas Magharibi, Ziwa Almas Mashariki, Ziwa Elucio, na Ziwa Allure) vile vile, kuna jumba la JLT la 8 linalotazamana na visiwa vya Jumeirah. Maziwa haya (ambayo ni mita 3 kwenda chini) maziwa haya yalijazwa kabisa mwisho wa mwaka 2009. [1] Jumla ya eneo lililofunikwa na maziwa, njia ya maji na ardhi itakuwa mita za mraba 730,000. Majumba yatakuwa na maghorofa mbalimbali, kutoka 35 hadi 45, isipokuwa lile la kati ambalo litakuwa na ghorofa 66. Jumba refu kabisa na lile maarufu kabisa katika eneo hili litakuwa [Almas Tower] ambalo litakuwa katika kisiwa chake pekee kati ya Ziwa Almas Magharibi na Ziwa Almas Mashariki. Majumba yote ya makazi yatakuwa katika makundi matatu. Hili litarahisisha usambazaji wa barua.
Ukamilishaji wa mnara wa Saba mwezi Desemba 2006 uliadhimisha jumba la kwanza kukamilika katika minara ya ziwa Jumeirah. Jumba la mwisho linatarajiwa kukamilika mwaka 2011. Ujenzi kwa kiasi kikubwa ulifinyika mwaka 2008.
Mwezi Oktoba mwaka 2008 jumla ya majumba 19 yalikuwa tayari kutumika na mengine 6 yalifunguliwa mwishoni mwa mwaka 2008.