Mitindo

Kufuata Fasheni (1794), katuni ya James Gillray.
Mwanamitindo nchini Tanzania

Mitindo (au fasheni kutoka Kiingereza fashion) ni njia ya mtu, kundi au jamii kufanya au kuwasilisha jambo kwa namna maalumu. Kwa mfano kufanya jambo harakaharaka, polepole, kwa taratibu fulanifulani na kadhalika. Halafu hiyo namna maalumu inaenea katika jamii, hasa upande wa mavazi. Mitindo inabadilikabadilika kadiri ya mahali na nyakati.[1][2][3]

Kuna watu maalumu ambao wanabuni mitindo mipya, wanaionyesha na kuisambaza, mara nyingi kwa faida kubwa kiuchumi.

Kutokana na utandawazi, siku hizi mitindo inaenea duniani kote, hasa kutoka nchi tajiri kwenda nchi maskini, na pengine inaharibu maadili na utamaduni.

  1. Fashion (2012, March 29). Wwd. (n.d.). Retrieved from http://www.wwd.com/fashion-news.
  2. Undressing Cinema: Clothing and identity in the movies – Page 196, Stella Bruzzi – 2012
  3. For a discussion of the use of the terms "fashion", "dress", "clothing", and "costume" by professionals in various disciplines, see Valerie Cumming, Understanding Fashion History, "Introduction", Costume & Fashion Press, 2004, ISBN 0-89676-253-X

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne