Mjane ni mtu aliyewahi kuwa na mwenzi wa ndoa, halafu akafiwa asioe tena ama asiolewe na mwingine.
Ni tofauti na yule asiyewahi kufunga ndoa (ambaye anaweza kuitwa vizuri zaidi mseja au, akiwa mwanamume, hata kapera, ingawa jina hilo la mwisho pengine linaelekea uhuni kidogo) na yule aliyetoa ama kupata talaka (anayeitwa mtaliki).