Mji ni mkusanyiko wa makazi ya watu, shule, hospitali, ofisi, maduka, viwanda n.k. ulio mkubwa kuliko ule wa kijiji. Mji ukizidi kukua unakuja kuitwa pia jiji.
Sura maalumu ya miji inategemea mambo mengi, kuanzia mazingira asili (kama yana milima, mabonde, mito, bandari n.k.).
Miji ya kwanza ilipatikana Mesopotamia, kama vile Uruk na Ur, ingawa kati ya miji inayodumu hadi leo ule wa kale zaidi labda ni Yeriko (Palestina).
Ukuaji wa madola ulifanya baadhi ya miji ipewe hadhi ya mji mkuu, kama vile Roma ambao wakati wa Yesu ulikuwa na wakazi zaidi ya nusu milioni.
Miji yenye wakazi wengi kuliko mingine ni Chongqing, Tokyo, Shanghai, Jakarta, Faiyumna na Varanasi n.k.
Africa ina miji mingi muhimu: Cairo, Lagos, Kinshasa, Johannesburg n.k.