Mkoa ni eneo fulani ndani ya nchi ambalo ni ngazi ya utawala wa nchi ile.
Matumizi ya jina hilo yanaweza kuwa tofauti kati ya nchi na nchi. Kwa kutafsiri vitengo vya utawala vya nchi mbalimbali wakati mwingine kuna mchanganyiko wa maneno "mkoa", "wilaya" na "jimbo" hasa kwa sababu matumizi ya maneno yanayolingana kwa ya Kiingereza "region", "district" na "province" hayafuati kila mara utaratibu maalumu.