Mkoa wa Kagera

Mkoa wa Kagera
Mahali paMkoa wa Kagera
Mahali paMkoa wa Kagera
Mahali pa Mkoa wa Kagera katika Tanzania
Majiranukta: 1°55′S 31°18′E / 1.917°S 31.300°E / -1.917; 31.300
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Mji mkuu Bukoba
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Meja General Marco Gatitu
Eneo
 - Jumla 40,838 km²
 - Kavu 28,953 km² 
 - Maji 11,885 km² 
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 2,989,299
Tovuti:  http://www.kagera.go.tz/
Mandhari ya Kagera.

Mkoa wa Kagera kati ya mikoa 31 ya Tanzania ndio mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa wenye postikodi namba 35000. Jina lake linatokana na mto Kagera.

Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mingine ya Tanzania, yaani Kigoma, Shinyanga na Geita.

Eneo lake ni km² 28,953 za nchi kavu na km² 11,885 za maji ya ndani, hasa ya Viktoria Nyanza, jumla km² 40,838.

Mkoa wa Kagera uko mnamo mita 1000 juu ya uwiano wa bahari.

Makao makuu ya mkoa ni mji wa Bukoba.

Kiutawala eneo la mkoa limegawiwa kwa wilaya nane: Bukoba, Misenyi, Muleba, Karagwe, Ngara, Biharamulo na Kyerwa pamoja na manisipaa ya Bukoba. Misenyi ni wilaya mpya iliyoanzishwa mwaka 2007 na Kyerwa ikafuata mwaka 2012.

Sensa ya mwaka 2022 imeonyesha idadi ya wakazi kuwa 2,989,299 inayoendelea kuongezeka kasi [1].

Mkoa huu una makabila makubwa manne ambayo ni Wahaya, Wanyambo, Wahangaza na Washubi. Wahaya huishi kwa wingi katika wilaya za Bukoba, Muleba na Misenyi, Wanyambo huishi kwa wingi katika wilaya za Kyerwa na Karagwe, Wahangaza huishi kwa wingi katika wilaya ya Ngara, na Washubi huishi kwa wingi katika wilaya ya Biharamuro.

Makabila ya Wanyambo na Wahaya hupenda kula ndizi kwa wingi na asilimia kubwa wanafuata mila na desturi za mababu: zamani Wanyambo na Wahaya walikuwa hawawezi kuoana na hiyo bado sasa ipo kwa kiasi kidogo.

Pia mkoa huo una wakimbizi wengi, kwa asilimia kubwa wanatokea nchi za Rwanda na Burundi wakipitia wilaya ya Ngara.

  1. https://www.nbs.go.tz

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne