Mkoa wa Kilimanjaro |
|
Mahali pa Mkoa wa Kilimanjaro katika nchi ya Tanzania | |
Majiranukta: 3°20′S 37°20′E / 3.333°S 37.333°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 7 |
Mji mkuu | Moshi |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | |
Eneo | |
- Jumla | 13,209 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,861,934 |
Tovuti: http://www.kilimanjaro.go.tz/ |
Mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 25000.
Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kupita yote barani Afrika, umo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Jina la mlima huu ndilo limeupatia mkoa jina lake.
Mkoa wa Kilimanjaro umepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa kusini na mikoa ya Manyara na Arusha upande wa magharibi.